- Taarifa Binafsi โ Weka jina lako kamili, barua pepe, na namba ya simu.
- Uthibitisho (OTP) โ Ikiwa ulishawahi kutumia Numi, namba ya siri itatumwa kwenye barua pepe yako ili kurejesha data zako.
- Mapendeleo โ Chagua sarafu unayotumia (TSh) na mitandao unayotumia (M-Pesa, Tigo Pesa, CRDB, n.k.).
- PIN ya Ulinzi โ Weka namba ya siri (PIN) ya tarakimu 4. Unaweza pia kuwasha alama ya kidole (Biometric).
๐ก Mfano:
Ikiwa jina lako ni "Juma", weka barua pepe juma@email.com na uchague sarafu ya TSh. Kisha tengeneza PIN yako ya siri kama 1234.
Jumla ya Salio โ Kiasi cha fedha kwenye mifuko yako yote. Bonyeza icon ya jicho kuficha.
Kadi za Mifuko โ Inaonyesha salio la M-Pesa, Tigo Pesa, Benki kwa haraka.
Vitendo vya Haraka โ Vitufe vya kuongeza miamala, bajeti, madeni, na ripoti.
Miamala ya Hivi Karibuni โ Orodha ya matumizi au mapato yako ya mwisho.
๐ก Mfano:
Dashibodi enaweza kuonyesha una TSh 500,000 kwa ujumla. Chini yake, unaona TSh 200,000 ziko M-Pesa na TSh 300,000 ziko Benki.
- Chagua Aina โ Bonyeza "Lipa" kwa matumizi au "Pokea" kwa mapato.
- Weka Kiasi โ Andika kiasi cha fedha, mfano 10,000.
- Chagua Jamii โ Chagua kama ni Chakula, Usafiri, Bili, au Burudani.
- Maelezo/Risiti โ Andika muamala huu umefanyika kwa nani na piga picha ya risiti.
๐ก Njia ya SMS: Nakili ujumbe wa SMS kutoka M-Pesa au Benki na kuupaste kwenye tab ya "SMS". Numi itasoma kiasi na mtoa huduma moja kwa moja!
๐ก Mfano:
Umenunua chakula cha mchana kwa TSh 5,000. Fungua "Add Transaction", chagua "Pay", weka 5,000, chagua jamii ya "Chakula", kisha Save.
- Kutoka (From) โ Chagua mfuko unamotoa fedha (mfano: Benki).
- Kwenda (To) โ Chagua mfuko unakopeleka fedha (mfano: M-Pesa).
- Kiasi โ Weka kiasi unachohamisha na bonyeza "Kamilisha Uhamisho".
๐ก Mfano:
Umetoa TSh 50,000 kwenye akaunti ya CRDB na kuziweka kwenye M-Pesa. Numi itapunguza salio la Benki na kuongeza salio la M-Pesa kwa wakati mmoja.
Weka Bajeti โ Pangia kila jamii kiasi chake (mfano Usafiri: TSh 50,000 kwa mwezi).
Ufuatiliaji โ Numi itakuonyesha asilimia ngapi umetumia na kiasi gani kimebaki.
Tahadhari โ Rangi itabadilika kuwa njano au nyekundu ukikaribia kuzidisha bajeti.
๐ก Mfano:
Umejipangia bajeti ya TSh 100,000 kwa Bili. Ukishalipia TSh 80,000, Numi itakuonyesha umetumia 80% na imebaki TSh 20,000.
- Kuongeza Deni โ Bonyeza "+" kwenye screen ya Debts. Andika jina la mtu, kiasi, na aina ya deni.
- Kupunguza Deni โ Bonyeza deni husika kisha chagua "Add Payment" kila unapofanya malipo.
- Historia โ Angalia kila tarehe uliyolipa na kiasi kilichobaki.
๐ก Mfano:
Umemkopesha Anna TSh 20,000. Akikulipa TSh 10,000, unaongeza malipo, na Numi itakuonyesha Anna sasa anadaiwa TSh 10,000 pekee.
- Lengo Jipya โ Bonyeza "Add Goal" na uweke jina, kiasi unacholenga, na icon unayopenda.
- Kuweka Akiba โ Bonyeza kadi ya lengo lako na uchague "Add Saving" kila ukiweka fedha.
- Mifuko โ Ainisha kama akiba iko kwenye Cash, Benki, au M-Pesa.
๐ก Mfano:
Una lengo la TSh 400,000. Kila mwezi ukiweka TSh 50,000, Numi itakuonyesha progress bar ikisogea mpaka ufikie 100%.
Ripoti โ Chati zinazoonyesha unatumia wapi pesa nyingi zaidi (40% Chakula, 20% Usafiri, n.k.).
Export โ Toa data zako kwa mfumo wa Excel (CSV) au PDF.
Maarifa (Insights) โญ Premium โ Ushauri wa AI kuhusu jinsi ya kuokoa fedha zaidi.
Bajeti ya Otomatiki โ Numi itakutengenezea bajeti kulingana na kanuni za 50/30/20.
Risiti Zisizo na Kikomo โ Hifadhi risiti nyingi uwezavyo bila kikomo.
Smart Insights โ Ushauri wa kina wa AI kuhusu matumizi yako.
Cloud Backup โ Data zako zitahifadhiwa mtandaoni. Hata ukipoteza simu utazikuta.
Kubadilisha Lugha (Kiswahili / Kiingereza)
Kuona Sarafu yako (imewekwa wakati wa usajili)
Kubadilisha PIN ya ulinzi
Kushirikisha programu na marafiki
Kusimamia mitandao yako (Providers)